HOT News

CHAMA CHA MAPINDUNZI WILAYA YA BUTIAMA CHAWAPIGA MSASA VIONGOZI WAPYA WALIOCHANGULIWA KATIKA NGAZI YA MASHINA NA MATAWI.

 


CHAMA CHA MAPINDUNZI WILAYA YA BUTIAMA CHAWAPIGA MSASA VIONGOZI WAPYA WALIOCHANGULIWA KATIKA NGAZI YA MASHINA NA  MATAWI.

 

Na Mwandishi wetu,

Ikiwa chama cha mapinduzi kikiwa kinaendelea na uchaguzi wa ndani ya chama katika ngazi mbalimbali kuanzia   mashina mpaka taifa,katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya butiama ndugu Hamisi Mkaruka Kura,aliandaa semina ya siku moja kwa viongozi wapya waliokwisha chaguliwa katika ngazi ya mashina na matawi ambao ni wenyeviti,makatibu na makatibu waenezi lengo likiwa ni kuwajengea uwezo viongozi hao namna ya kunadi ilani ya chama cha mapinduzi na kuendelea kudumisha umoja ndani ya chama.

 

Aidha  Mbunge wa Jimbo la Butiama Mh Jumanne Sagini ameshiki katika semina hiyo nakuwaomba viongozi hao kufanya kazi kwa uweledi na kuondokana na makundi ya ndani ya chama na kuyasemea maendeleo yanayofanywa na serikari chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambae pia ni mwenyekiti wa  chama cha mapinduzi Taifa.

 

 

Pia Mbunge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha na kuendeleza miradi ya maendeleo mengi yenye tija na yanayosaidia kuleta huduma kwa wananchi wa jimboni humo.

 

Sagini alieweza kutaja baadhi ya maendeleo yaliyotekelezwa na yanaendelea kutekelezwa kuwa ni;- Afya,Elimu,Maji na Barabara,ambapo ameishukuru serikali kwa kutoa pesa nyingi ndani ya jimbo hilo ambazo zimeweza kukamilisha baadhi ya miradi iliyokuwa  kitendawili kukamilika.

“Niliguswa sana  kuja kugombea nafasi ya ubunge Butiama baada kuona wakati nikiwa RAS Simiyu nilishudia tukijenga miradi mingi na inakamilika kwa wakati lakini niliumia sana kila nikija huku kwetu Butiama miradi inasuasua na mingine ipo kwenye mpango lakini haipati muafaka wa kuanza kutekelezwa  kwa wakati mf;- ujenzi wa Hospital ya Wilaya ilikuwa  imeshindikana kujengwa kutokana na mvutano wa baadhi ya watu kutaka ijengwe katika maeneo yao lakini Mimi nilimuomba mama Maria Nyerere akatupatia eneo la kutosha kujenga hosptali na Rais Samia kupitia fedha za uviko alitupatia pesa za kutosha na sasa ujenzi wa hospital hiyo uko umekamilika tunakamilisha mambo madogo madogo ili wananchi wetu waanze kupata huduma”

Hata hivyo aliendelea kuwasisistiza viongozi hao kuacha makundi na kushikamana kwa pamoja ili kuweza kufanya kazi kwa maendeleo zaidi ndani ya jimbo la Butima.

 

Pamoja na hayo pia katibu wa chama wilaya ya butiama aliwasihi viongozi hao kufanya vikao vya mara kwa mara katika maeneo yao kuyasemea yale ambayo serikali inatekeleza  kupitia ilani ya chama na  kusema hatashindwa kumchukulia hatua kiongozi aliechaguliwa na wanachama na akashindwa kutekaeleza majukumu yake atamuwajibisha kwa kufuata  kanuni za chama.

 

Hakuna maoni