MBUGE WA JIMBO LA BUTIAMA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AMSHUKURU RAISI SAMIA KWA KUTOA PESA ZILIZOSAIDIA KUKAMILISHA MIRADI NDANI YA JIMBO LAKE.
Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri Wa Mambo Ya Ndani, Jumanne Sagini ametembelea miradi mbalimbali ya Elimu,Afya na Maji katika ziara yake inayoendelea Jimboni kwake na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassani kwa kutoa pesa za kutosha kukamilisha miradi hiyo iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.
Aidha Sagini
amewasihi wananchi Jimboni kwake kuendelea kujitolea kuanzisha miradi
mbalimbali na kusema kuwa ikotayari kushirikiana na wananchi wenye nia na
kulijenga taifa lao kimaendeleo.
Ujenzi wa zahanati ya kwigutu uliogharimu kiasi cha sh
million Hamsini 5000000/= kutoka serikali kuu aidha mbunge awapongeza wananchi
kwa jitihada zao za kuanzisha ujenzi wa zahanati hii.
Mbunge akikagua ujenzi wa zahanati ya Isaba iliyopo kata Buruma,iligharimu kiasi cha shilingi million Hamsini kutoka serikali kuu.
Sambamba na hayo mbunge alimsainisha mkataba mkazi wa Kijiji cha
Nyasirori bw;Mabigi Athumani Mabigi aliejitoa kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa
kisima cha maji kwa manufaa ya jamii,nakuwasihi wananchi wote kujitolea katika
maendeleo.
Mwisho mbunge aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa katika Sensa ya watu na Makazi kwa manufaa ya maendeleo ya Taifa letu.
FOR MORE INFORMATION VIST US YOUTUBE AS NEVILLA DIGITAL TV
Hakuna maoni