NETHEFOTA FURAHA YA WATOTO WENYE UHITAJI MKOA MARA.
Shirika la Nethefota ni shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kuwasaidia watotowenye mahitaji muhimu ya shule,Afya,Chakula ndani ya Mkoa wa Mara, ambapo mpaka sasa wamegusa maisha ya watoto zaidi ya Mia Moja kwa kila mmoja kutoka na uhitaji wake na wengine kuwasimamia katika matibabu kutoka na maradhi sugu yaliyokuwa yakiwasumbua.
Kuelekea msimu huu wa Sikukuu za kufunga na kufuangua mwaka, zinazoambatana na muendelezo wa maandalizi ya Watoto kurejea Mashuleni Shirika hilo limewatimizia mahitaji ya Shule Watoto Mia moja Hamsini (150),kwa kuwakabidhi BEGI,DAFTARI,COUNTERBOOK, RIM PARER,KALAMU NA MIKEBE,zoezi hilo limewagusa Watoto kutoka shule mbalimbali za Wilaya ya Musoma Mjini Na Wilaya ya Butiama ndani ya Shule za Msingi, na wale wanaotarajiwa kujiunga Kidato cha kwanza mwakani 2024.
Mkurugenzi wa shirika hilo Bwana Patricki Jaraba,amesema
shirika la Nethefota linayomalengo makubwa zaidi na enderevu kwa ajili ya
kuwasaidia watoto kwa kila hali watakavyojaaliwa ili kushirikiana na Serikali
kulijenga Taifa lililo imara katika misingi bora ya Elimu kwa mtoto na kuwasihi
Wazazi wa Watoto hao waliohudhulia katika zoezi hilo kuhakikisha wanawasimamia
Watoto vyema kuhudhulia Masomo na kuwalea kiroho katika njia za kumpendeza
Mungu na kuwakumbusha Watoto wasijihusishe na makundi mabaya yanayoweza
kuwaingiza hatarini na wakashindwa kutimiza ndoto zao.
Hafla hiyo ilihudhuliwa na Afisa maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mara, Bi Neema Ibamba,ambapo alitoa pongezi za dhati kwa Mkurugenzi wa shirika hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya kuunga mkono Serikali katika Sekita ya Elimu kwa kuhakikisha watoto wenye uhitaji wanapata mahitaji ya Msingi na kuwasihi Wazazi na Walezi kuhakikisha hawakwamishi juhudi la shirika hilo kwa kusimamia malezi bora kwa Watoto kwa Dunia imeingiwa na mitindo mingi ya kimaisha ambayo ni hatari na inadhoofisha nguvu kazi ya vijana endapo wakikosa uangalizi wakatumbukia huko wakiwa bado wadogo wanapoteza Dira ya Maisha.
Mungu azidi kubarikiwa
JibuFuta