HOT News

SIJUI KUSOMA NA KUANDIKA BAADA YA MAMA KUFARIKI NIKAWA NA JUKUMU LA.........

 Celina Willium, Ni binti mwenye umri wa miaka kumi na nne anasoma katika shule ya msingi INGRI JUU iliyopo Wilayani RORYA  kupitia elimu ya watoto walio nje ya mfumo rasimi maarufu kama MEMKWA.

Celina alifiwa na mama yake akiwa na umri wa miaka tisa 8  na kumlazimu yeye kubaki kumlea mdogo wake kwa kuhakikisha anampa huduma za chakula,kuoga n.k, kwani mama yake alipoteza uhai wakati wa kujifungua na kumuacha mdogo wake akiwa masaa matatu duniani.

"Napenda sana kusoma na natamani nijue kusoma na kuandika kama wenzangu ila nashindwa kutokana na mazingira magumu ya  nyumbani kwetu,kwani nilifiwa na mama yangu mzazi na ikanilazimu nikae nyumbani kwa muda mrefu nikimlea mdogo wangu alieachwa na mama yangu akiwa na masaa kadhaa duniani hivyo ilisababisha nishindwe kuhudhuria shule kila siku.

Maisha yalibadilika baada ya mama kufariki Baba alioa mwanamke mwingine ambae akawa ni mama yetu mdogo alijitoa kwa kila hali kuhakikisha nahudhulia shule,Baada ya muda Baba yangu mzazi alipatwa na ugonjwa wa Kwikwi ulimtesa kwa miezi kadhaa kutokana na kukosa huduma  Baba yangu alipoteza uhai pia.

Baba yangu alikuwa anafanya kazi katika kiwanda flani cha soda huko Mwanza ila alizurumika pesa zake pengine angeweza kupata huduma  ila ilishindikana na mapaka akafariki.

Maisha yalizidi kuwa magumu baada ya baba kufariki tulibaki na mama yetu wa kambo mpaka sasa anajitahidi sana nisome ila changamoto inakuwa ni mimi kupata mahitaji muhimu ya shule kuna muda nakosa Viatu,Sale za Shule,Daftari na kalamu ila pale ninapofanikiwa kupata nahudhulia shuleni  na  kutokana na kuwa mtoro mara kwa mara imenifanya mpaka sasa sijui kusoma na kuandika vizuri zaidi ya kujua kuandika jina langu na la mzazi wangu"Amesema Celina.

Hayo yamebainika baada ya timu ya utekelezaji  wa maradi wa  RUDI SHULENI  (BACK TO SCHOOL)unaotekeleza mradi wa MEMKWA baada  kutembelea shuleni hapo wakiwa na viongozi wa elimu Serikalini ngazi ya Wilaya na Mkoa kutoka Mkoani Mara kwa ajili ya kukagua maendeleo ya kituo hicho ndipo walipobaini changamoto ya binti Celina na kuahidi kuendelea kumsaidia zaidi yeye na mdogo wake ambae kwa sasa nae alipaswa awe ameanza shule ila kutokana na familia kukosa uchumi haijawezekana kumpeleka shuleni.


Mradi wa RUDI SHULENI (BACK TO SCHOOL)  (MEMKWA) Unatekelezwa na Graca Machel Trust kutoka Africka Kusini  kwa kushirikiana na Jimbo katoliki la Musoma Mkoani Mara.


Hakuna maoni