GHATI CHOMETE APIGA JEKI WANAWAKE VIKUNDI 16.
Na Neema Kobiro
Mbunge viti maalum mkoa wa mara Mh Ghati Chomete apiga jeki vikundi kumi na sita 16 mkoani mara kwa kuwafungulia akaunti benki lengo likiwa kuwawezesha kupata mikopo inayotolewa na Halmashauri jambo ambalo vikundi hivyo walishindwa kulikamilisha kwa muda mrefu.
Zoezi hilo amelitekeleza kupitia ziara ya Naibu katibu mkuu UWT Taifa inayoendelea mkoani Mara na kuwasihi wanawake hao wawe na umoja mtulivu katika vikundi vyao na kuweka mipango madhubuti ya matumizi ya pesa hizo ili kujiendeleza kiuchumi.''Wanawake wenzangu mimi nawawezesha kwa kuwafulia akaunti ili muweze kukopesheka pesa zinazotolewa na Halmashauri zetu kwa lengo nanyi muweze kujikwamua kiuchumi,tumieni frusa za pesa za mikopo zinazotolewa kwa manufaa ya taifa letu na jamii kwa ujumla epukeni kuchukua pesa hizi na kwenda kuzitumia katika matumizi yasiyo sahihi na baadae kushindwa kuziresha na nina imani mtaenda kuzifanyia kazi kikamilifu na umoja wa vikundi vyenu utadumu zaidi na kupata maendeleo,Alisema Ghati''
Aidha mbunge aliendelea kwa kuwasisitiza wanawake mkoani Mara waendelee kuunda vikundi kwa wingi kwani serikali kupia Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani imekusudia kuwainua wanawange wote kiuchumi katika ngazi zote hivyo ni vyema kuonyesha mwitikio katika kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo itayowawezesha kurejesha pesa hizo ili na wengine pia wakopeshwe.
Pia mhe Ghati amewaomba wanawake wote kuwa wasimamizi wakuu kwa kuhakikisha zoezi la sensa ya watu na makazi likanakamilika kikamilifu katika kaya na jamii kwani wanawake siku zote ndio watu makini kwa ukamilifu wa mambo yote ya kifamilia na kuwambusha kutoa taarifa sahihi za idadi ya watu walionao kwa kuzingatia maswali ya makarani wa sensa wataopita katika kaya zao.
Pamoja na hayo amewakumbusha wanawake kupitia sensa serikali itaweza kukamilisha mahitaji mengi muhimu ya kijamii kwa kutambua idadi ya wanachi wao ikiwemo na kuongeza fungu la pesa za mikopo ya akina mama,makundi maalum pamoja na Vijana hivyo wasiwafiche ndani watu wenye ulemavu wa aina yoyote kwani serikali inatambua uwepo wao na inatoa fungu kwa ajili yao hivyo ni vyema kutoa idadi sahihi ili na wao waongezwe katika bajeti.
Hakuna maoni