''WAKAMATWE WOTE WALIOHUSIKA NA MAUAJI''NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI SAGINI.
Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama mh Jumanne Sagini, ameliagiza Jeshi la polisi mkoani mara kuawasaka watuhumiwa wote waliohusika na mauaji ya mzee Omary Iyombe mkazi wa kitongoji cha kwigina kijiji cha kizaru kata ya Muriaza wilayani Butiama,Baada ya kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali kichwani wakati akipita kutoka sokoni na kuwakuta baadhi ya familia walio na mgogoro wa aridhi wakizozana na kumvamia nakuanza kumjeruhi jambo lililopelekea kupatwa na mauti.
Akizungumza na wananchi wa kijijini hapo mhe Sagini, amewataka wanachi hao kufuata taratibu na sheria za nchi kutatua migogoro inayowakabili na si kujichukulia sheria mikononi na kupelekea kupoteza uhai wa mtu kwani hii inapunguza nguvu kazi kwa Taifa na Jamii kwa ujumla.
Aidha Naibu waziri Sagini amewaomba watumishi wauma kuepuka kuuza Aridhi ya mashamba ya bega kwa bega yaliyokuepo tangu enzi za mwalimu J.K Nyerere kwani uwepo wa mashamba hayo utaendelea kusaidia jamii kujenga shule,zahanati na hata kuweka masoko,
''Niwashauri watumishi wa Uma jaribuni kuepukana na tamaa ya vitu vidogovidogo na badala yake kuweni na moyo wa kulinda rasilimari mnzozikuta kwa maendeo ya nchi yetu''Hayo ameyasema kufuatia mgogoro wa mipaka ya aridhi uliopo baina ya kijiji cha Kizaru na Kamgendi ambao ndio unaotajwa kuwa chanzo cha mauaji ya mzee Omary Iyombe.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Kenedi Juma, ameomba serikali kutatua matatizo ya migogoro ya aridhi kwa wakati kwani mgogoro wa mipaka kati vijiji hivyo viwili ni wa muda mrefu ni takribani miaka thelathini na mitano (35) na imeshasababisha maafa ya kuwapoteza ndugu zao wawili Mwita machele alieuwaa mwaka 2017 na sasa wamempoteza Omary Iyombe huku wakiwa hawana amani, na vijiji hivi iwili hawawezi kushirikiana kwa haliyoyote ya kimaendeleo na hata kufungiana njia za kupita hali inayozidi kuwatia hofu wananchi hao na kubaki na sintofahamu licha ya kuwa uongozi wa Wilaya wanayo taarifa ila imekwishakuwa ni kitendawili kutatua mgogoro huo.
Pamoja na hayo Naibu Waziri amemuagiza mkuu wa wilaya ya Butiama pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Butiama kuhakikisha wanatatua mgogoro huo kwa masilahi ya wananchi na Serikali kwa ujumla,na kuwaomba wananchi kuendelea kuwa wavumivu katika kipindi hiki ambapo Jeshi la polisi likishughulika kuwasaka wale wote waliojihusisha na mauaji hayo.
''Niwatoe hofu mimi kama muwakilishi wenu Mbungeni na Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nitahakikisha tatizo hili linapata ufumbuzi kwa haraka na Tanzania yetu ni nchi ya amani hivyo yeyote atakaejihusisha na kuwazuia wananchi wenzao kufanya maendeleo katika kijiji chochote ndani ya kata hii na kuzuia watu wa eneo flani wasipite kuelekeo eneo jingine tutawadhibiti hivyo ninaomba kuanzia sasa matendo ya unyanyasaji yafutike''alisema Sagini.
Hakuna maoni