HOT News

WANAWAKE UWT SERENGETI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI WAONGEA NGUVU SENSA YA WATU NA MAKAZI.



Wanawake Wilayani Serengeti kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameandaa kongamano la   kuhamasisha Sensa ya watu na makazi Wilayani humo lengo likiwa ni kuwaelimisha wakazi wa wilaya hiyo   nini  maana  ya Sensa  na umuhimu wake kwa maendeleo yao.

Akizungumza katika kongamano hilo katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa mara Langaeri Akyoo ambae ndie aliekuwa mgeni rasmi amewaomba wananchi kuondoa hofu juu ya zoezi la sensa na kuyapuuza mambo ya upotoshwaji yanayovumishwa mitaani na watu wachache kwani lengo la serikali ni kutaka kupata takwimu halisi za Watanzania kwa ajili ya kutoa huduma za kimaendeo ndani ya  Taifa letu.

Pia katibu alitoa malengo ya serikali juu ya sensa ni kutaka kutoa huduma bora katika sekta zote ndani ya nchi yetu ikiwemo na wilaya ya Serengeti kwani bila kupata idadi kamili ya wakazi wa eneo husika Serikali haiwezi kutoa kiwango cha huduma toshelevu kutokana kutoelewa idadi ya wakazi wa eneo tajwa  na  kupitia zoezi la  Sensa Serikali itapata  takwimu kamili kila mwananchi atanufaika na huduma zitakazotolewa na Serikali .


Aidha katibu wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT mkoa wa Mara, Bi Mariam Iddi, amewaomba wanawake kujitokeza kwa wingi katika zoezi la sensa ya watu na makazi na kuwatoa idadi halisi ya watu wote walioko katika kaya zao na kuwaomba viongozi wa kata zote ndani  ya  UWT wilaya ya serengeti kuendelea kutoa elimu juu sensa ya watu na makazi ili wanachi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa. 

Hata hivyo Bw Akyoo  alihitimisha kwa kuwakumbusha wananchi kuwa makarani wa sensa wamepewa semina yakutosha juu ya kazi ya ukusanyaji wa takwimu  katika kaya zetu  na watauliza maswali ya msingi na yenye tija na wataongoza na wenyeviti wa mtaa au kijiji na hakutakuwa na ubabaishaji  hivyo ni vyema kuwapa ushirikiano mzurikwa kujibu maswali vyema  kutokana na watakayoouliza na kuwaomba wasiwafiche idadi za watu wote hata kama ni mlemavu anayo haki ya kuhesabiwa.





Hakuna maoni