HOT News

''WALIMU MKO MIKONO SALAMA'' NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI SAGINI.

Na Neema kobiro
Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi na mbunge wa jimbo la Butiama Jumnne sagini amewaondoa wasiwasi  waalimu wa wilaya ya Butiama waliokuwa na hofu ya kiutendaji kufuatia mauaji ya Mwalimu Saidi Saidi Hamisi,aliekuwa akifundisha shule ya sekondari Masaba iliyopo wilayani humo mkoani Mara.

Akizungumza katika kikao cha  kufanya Tathimini ya maendeleo ya elimu ya sekondari katika wilayani Butiama na kutoa vyeti na zawadi mbalimbali kwa walimu wanaofanya vizuri kiufundishaji na shule zilizoongoza kiufaulu amesema mauaji ya Mwl Said Said Hamisi  hayatafasiri kuwa wananchi wa Butiama wana chuki na Walimu bali wahalifu waliotenda tukio hilo walienda kumvamia kwa malengo ya kupata masilahi binafsi kutokana na kwamba mwalimu huyo nje ya ualimu alikuwa mfanyabiashara

Mhe Sagini aliendelea kwa kuwaomba Maafisa Elimu ngazi zote pamoja na waalimu wakuu wote kuepuka kuwa chanzo cha maambukizi ya hasira yanayoweza kusababisha  kushuka kwa kiwango cha Elimu kwa watoto mashuleni, ''Epukeni kuwatendea mabaya watu wa chini yenu kwa kutumia nafasi zenu za kiuongozi  na hata ikitokea umeumizwa epuka kuhamisha hasira mf;Afisa elimu ngazi ya wilaya anamkwaza Afisa elimu kata, Afisa Elimu kata unahama na Hasira zako kwenda kwa Mkuu wa shule, Mkuu wa shule  anaenda kumkomesha mwalimu wa kawaida  na mwalimu anamkomoa mwanafunzi sasa kwa cheni hii anaeumizwa ni mwanafunzi naombeni sana tuweni na umoja ili tupandishe kiwango cha ufaulu kwa watoto wetu''amesema Sagini.

Pia  ametoa pongezi kwa Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Butiama Chacha Megawa  kwa utendaji kazi bora  jinsi avyozidi kuujenga umoja kwa  waalimu ili kuondoa ziro mashuleni hii inaonyesha ishara ya matokeo mazuri ya mitihani mbeleni na kuongeza kuwa yeye kama muwakilishi wa wananchi hayuko tayari kukubaliana na mtu yeyote atakaetaka kuvunja muungano waliouanzisha wa kukuza ufaulu kwa watoto kwa ngazi zote za msingi na Sekondari.

Hakuna maoni