''WASHEHEREKEE WAKIWA MIKONONI MWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA HAIWEZEKANI''
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi ambae ni Mbuge wa Butiama Mh Jumanne Sagini ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama Wilayani Butiama kuwasaka waharifu wote wanaojaribu kutaka kupoteza amani Wilayani humo msimu huu wa sikukuu.
Sagini ameyasema hayo Kata ya Bukabwa alipohudhuria hafla fupi ya pongezi, iliyoandaliwa na Baraza la Wazee kwa lengo la kumpongeza Rais, Mbunge na Diwani kwa namna walivyotatua changamoto za huduma za kijamii kwa kuzigusa sekta zote ndani ya Kata ya Bukabwa na Jimbo la Butiama kwa ujumla na kubaini uwepo wa kundi la watu waliojitokeza na kuibui tabia ya wizi wa Mifugo ya wananchi jambo linalopelekea kupoteza amani kwa msimu wa huu wa siku kuu za kufunga na kufungua mwaka.
Aidha Naibu Waziri alimtaka mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Amos Kitajo Sanga kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama Kata ya Bukabwa kwa kushirikiana na wananchi bila kujali uzao,undungu au ukabila wasisite kuwataja wale wote wanaosadikika kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Nae Mwenyekiti wa kijiji hicho ameonyeshwa kukerwa na kukemea vikali vitendo hivyo na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha huku wanachi wa kijiji hicho kupaza sauti zilijaa hasira na kuifurahia kauli iliyotolewa na Naibu Waziri na kusema watatoa ushikiano wa kutosha hata kama ni watoto wao au wanafamilia waliopo Majumbani mwao watawataja bila kusita.
Hakuna maoni