WANAFUNZI WAWILI WAPOTEZA MAISHA
Wanafunzi wawili wa shule ya msingi Nyasirori iliyopo kata ya Masaba Wilayani Butiama Emanuel Robert Shabani,miaka kumi na tano (15) darasa la saba,na Lameck Juma Wanzagi, miaka kumi na moja (11) darasa la nne wapoteza maisha wakiwa wanatoka shule na kwenda kuogelea katika dimbwi la maji mengi la Kuseka lililopo maeneo jirani na Nyumbani kwao.
Akizungumza na Nevilla Blog Mtendaji wa kijiji hicho Bw Paschal Mitagito amesema imekuwa nikawaida ya watoto hao kwenda kuogelea hapo hata wanapokuwa nyumbani kwani ni dimbwi linalopatikana maeneo jirani na makazi yao hivyo pia walizoea hata wanapotoka shule kwenda kuogelea dimbwini hapo.
Aidha aliendelea kwa kusema siku ya tukio lilikuwa ni kundi kubwa la wanafunzi waliokuwa wakiogelea moja ya wakazi wa maeneo hayo alienda na kuwazuia watoto hao na kuwaamuru waondoke kwenda nyumbani lakini vijana hao wawili walijificha na kurudi kuendelea kuogelea ndipo mmoja wapo alipozama na mwenzake kwenda kumuokoa lakini hakufanikiwa na kupelekea wote wawili kupoteza maisha.
Hata hivyo mtendaji amewaomba wazazi na walezi kuwa walinzi wa watoto kwa kuwatahadharisha kucheza katika mazingira hatarishi na kuwaomba wakazi wa kijiji hicho kufukia madimbwi yote na mashimo ambayo ni hatari kwa maisha ya watoto.
Hakuna maoni