HOT News

TAARIFA YA ZIARA WAJUMBE WASEMA NG'ONG'A HATUTAMUANGUSHA TUKO NAE BEGA KWA BEGA.

Mhe Ng'ong'a akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa halmashauri kuu  kata Rabour baada ya semina ya uongozi aliyoiandaa na kuendeshwa na katibu wa chama cha mapinduzi Bw Nathon Manyonyi katika ukumbi mdogo wa chama cha mapinduzi  ndani ya ofisi za chama  mkoa,huku wajumbe hao wakiifurahia semina hiyo kwani imezidi kuwaimarisha kiutendaji katika kipindi chote watakachokuwepo madarakani na kuomba isiwe mwisho wa wao kupewa darasa la uongozi.



Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Rolya na diwani wa kata ya Rabour  mh Gerald Ng'ong'a akisaini kitabu kwa katibu wa chama cha mapinduzi wilayani Butiama kabla ya kuanza ziara yake na wajumbe wa halmashauri kuu kata ya Rabour kutembelea nyumbani kwa baba wa Taifa JK Nyerere.


Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Rolya  Nathon Manyonyi  akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya katibu wa chama wilaya ya Butima,ambae alikuwa mseminishaji  mkuu katika semina iliyoandaliwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rolya nae alipata frusa ya kwenda kutembelea nyumbani kwa baba wa taifa kupitia ziara ya Ng'ong'a .

Baada ya kuwasili Nyumbani kwa baba wa Taifa walipokelewa na mmoja wa wanafamilia hiyo tayari kwa kuanza kutembeza maeneo mbalimbali ili kujifunza maisha aliyoyaishi baba wa Taifa enzi za uhai wake.
Baada ya kupokelea walianza kutembelea ikiwemo na kufika katika makaburi ya wazazi wa Baba wa Taifa Mama na Baba yake 
Ukizitizama picha hizo za makaburi kwa umakini katikatiya makaburi hayo kuna alama ambayo haikuwekewa kigae kwa maelezo ya mwenyeji wetu alitueleza kuwa hiyo ni sehemu ya kufanyia mitambiko kutokana na imani ya kila mmoja .



Aidha wajumbe walifikishwa katika eneo makumbusho alipozaliwa baba wa taifa hapo ilipowekwa picha wa baba wa taifa ndipo ilipokuwepo nyumba ambayo baba wa taifa alimozaliwa hivyo iliwekwa picha hiyo kama kumbukumbu ya mahali pa kuzaliwa kwake.

Hapo ni sebleni kwa Baba wa Taifa na kiti alichokalia Mwenyekiti wa Halmashauri cha kushoto ndicho kiti alichopenda kukalia Baba wa Taifa na kulia alikaa Mkewe Mama Maria Nyerere.Na Nyumba hiyo imejengwa kwa mawe mwanzo mwa msingi mpaka boma isipokuwa paa pekee.


Kibanda cha mapumziko ya baba wa Taifa akiwa anacheza bao baada shughuli zake 
Baba wa taifa mbali na kuwa kiongozi alikuwa ni mkulima wa mazao ya ulezi na karanga hivyo alipokuwa akiwa shambani alikuwa anakuwa na jembe la ziada ukimtembelea shambani nawe atakupa jembe mkiwa manaendelea kuzungumza nawe utakuwa ukilima.
Hivyo  nao wajumbe walifurahia na kucheza bao kidogo huku wakizungumaza mawili matatu waliyojifunza kupitia utalii huo wa ndani.


Katika Nyumba hii ndimo lilimo kaburi wa baba wa taifa na wajumbe walilitembelea na kufanya sala fupi kumuombea baba wa Taifa aendelee kupumzika kwa Amani.

Pamoja na hayo ziara hiyo ilizaa matunda mazuri kwa wajumbe hao kwani wengi wao walikili kufurahia shule waliyoipata juu ya uongozi lakini pia kwenda kutembelea kwa baba wa taifa kwani wengi wao  hawakuwa kufikili kama ipo siku na wao watafika kwa baba wa taifa licha ya kuwa na wao ni wazawa wa Mkoa wa Mara,hivyo walitoa pongezi nyingi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Rorya ambae pia ni  Diwani wa kata ya Rabour kwani wamejifunza vitu vingi kupitia ziara hiyo na kumwahidi kutomwangusha kiutendaji na watakuwa nae bega kwa bega hatua kwa hatua katika kuitakeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

Hakuna maoni