MBUNGE ACHANGIA ONGEZEKO LA UFAULU MASHULENI TUNAKUSHURU UMEKUWA MFANO KWETU KIUTENDAJI.
Na Neema Kobiro
Akizungumza katika kikao cha kufanya Tathimini ya maendeleo
ya elimu sekondari Afisa elimu sekondari Wiliyani Butiama Bw Chacha Megawa
amempongeza mbunge kwa kuwa na mahusiano mazuri na walimu na kuanzisha
utaratibu wa vikao baina yake na walimu hali inayopelekea kuongezeka kwa
kiwango cha ufaulu mashuleni na kwa juhudi zake kuboresha miundombinu ya Elimu
na kusaidia upatikanaji wa waalimu mashuleni jambo ambalo linazidi kuwapa nguvu
wao kama viongozi na kusema hawatamuangusha watahakikisha Wilaya ya Butiama
inashika nafasi nzuri kiufaulu kwa ngazi ya Mkoa na hata Taifa.
Pia pamoja hayo alisema
wao kama vingozi wanayo mikakati Madhubuti waliyoiweka kwa kushirikiana na walimu
ilikuzidi kuongeza kiwango cha ufaulu 1,Kutoa
mazoezi ya ziada kila ijumaa ili kuwapatia fursa wanafunzi siku za wiki
kujisomea na kufanya mazoezi 2,kuendelea kutoa motisha kwa shule zinazofanya
vizuri pamoja na Walimu watakaokuwa wametoa ufaulu mzuri kwa somo husika
analofundisha na mbinu nyinginezo nyingi walizoziwekea kuhakikisha wanatokomeza
ziro.
Aidha aliendea kwa kuzitaja shule zilizoongoza kwa kufanya
vizuri kuwa ni; Chief Ihunyo,Busegwe sekondari,Buruma sekondari,Musoma utalii,Kukirango
sekondari na Bumangi sekondari na kuwasisistiza waalimu wa shule hizo waendelee kuongeza juhudi ili wasishuke
kiufaulu,pia alizitaja shule ambazo zimeongoza kwa kufanya vibaya kuwa ni
Bumaswa sekondari,Mirwa sekondari na Buhemba sekondari na kuwaagiza wakuu wa
shule hizo kuongeza juhudi na kusema kuwa wao kama viongozi hivi sasa
wataelekeza nguvu katika shule hizo na kuhakikisha wanatoa matokeo mazuri kwa
awamu zijazo.
Nao Waalimu walikuwa na malalamiko machache kwa baadhi ya viongozi
wa Halimashauri na Wilaya kwa kutowajali na kuwathamini pindi wanapoenda
kuwaona katika ofisi zao hawapati ushirikiano wa kutosha na hata kufedheheshwa
na kupata majibu yasiyo na tija hali
inayowapelekea kupoteza kujiamini kiutendaji.
Pamoja na hayo Mhe Sagini aliwashukuru kwa pongezi zao na
kuwahakikishia kuwa ataendelea kushirikiana nao hatua kwa hatua na hatafurahi
kuona mtu yeyote anajitokeza kutaka kukwamisha juhudi zao na kusema kuwa
atazidi kuongeza juhudi yeye kama Mbunge kuzidi kutafuta pesa Serikalini ili
kuzidi kuboresha miundombinu yote ya Elimu Wilayani humu ikiwemo na
kuwasisitiza wananchi kuendelea kujitolea kuanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kupunguza msongamano kwa Watoto Darasani na kwa shule zote zilizo
na hosteli pia atahakikisha wanafunzi wanafurahia kuishi mashuleni mwao.
Hakuna maoni