HOT News

TCCIA YAWEKA HISTORIA MARA.

Na Neema Kobiro.Naibu Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butima Jumanne Sagini atoa pongezi kwa viongozi wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo TCCIA Mkoani Mara  kwa kuandaa maonyesho ya Biashara yaliyowakutanisha wafanyabiashara mbalimbali ndani ya Tanzania kutoka Mikoa yote  katika uwanja wa Mkendo mjini Musoma, yenye lengo la kuutangaza mkoa wa Mara na pia ni sehemu ya vijana kujifunza ujasiliamali  na kuongeza pato kwa wakazi wa Musoma  na serikali kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari Sagini amesema licha ya kuwa ni mara ya kwanza kwa maonyesho hayo kufanyika mkoani Mara ila yamekuwa yakipekee kwani wameweza kujenga mabanda zaidi ya mia mbili 200 ambapo kila banda lina watu zaidi ya watatu   na kuwezesha  watu mia sita waliweza kuleta biashara zao katika mambanda hayo jambo ambalo linalotakiwa kuwa endelevu kwa kila mwaka ili kupunguza makundi ya vijana ambayo yanaweza kupelekea uhalibifu kwa taifa letu na badala yake waenda kupata ujuzi katika maonyesho hayo.

Aidha Mhe Sagini wakati akiendelea na zoezia la  ukaguzi wa mabanda hayo aliweza kutembelea banda la maliasili na utalii na kuwaomba kuwa mfano kwa kupanda miti na kuwafundisha wanchi namna ya kilimo bora cha misitu hususani  katika milima ya Kyanyari na Buturu inayopatikana Wilayani Butiama kama sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere na kuendelea kutunza mazingira ya nchi yetu, na kuongeza kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano wa hali juu kukamilisha zoezi hilo  kwa hali yoyote.

Pamoja na hayo amewaomba viongozi wa TCCIA  kuwa awamu ijayo na kuendelea nivyema yaandaliwe Wilaya nyingine kama sehemu ya kuleta chachu ya maendeleo ndani ya mkoa wetu isiwe Musoma mjini peke yake kwani lengo ni kuijenga Mara yenye uchumi mkubwa na kwa kupitia maonyesho hayo itasaidia kuleta maendeleo zaidi.

Hakuna maoni