ZAIDI YA BILIONI MBILI ZAPANUA MIRADI BUKABWA NA KUWATAMANISHA WANANCHI......
Mh Maswi ameyasema hayo katika hafla fupi iliyoandaliwa na Baraza la wazee wa Kata ya Bukabwa iliyohudhuriwa na viongozi wa chama ngazi ya Wilaya, Kata wakiwemo na viongozi wa Serikali ngazi ya kata na Wananchi wa Kata hiyo na maeneneo jirani, yenye lengo la kutoa pongezi kwa Chama na Serikali kwa namna wanavyojitahidi kuzitatua changamoto zilizokuwa na zinawakabili katika jamii.
Aidha Maswi amesema changamoto ya bwawa la maji ya mifugo Bukabwa lilikuwa ni kitendawili,
''Nilipambana sana kwa kipindi kilichopita kuweza kutatua changamoto ya bwawa la maji ya mifugo ila ilikuwa imekuwa ni kitendawili, nashukuru kwa kipindi hiki kupitia uzoefu wa Mbunge wetu tumepata Pesa kutoka Wizara ya mifugo Bwawa limekamilishwa na tumeweka miundombinu rafiki na ya kisasa kwa ajili ya kutibu mifugo yetu kama Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo,mradi uliogharimu zaidi ya Sh Milioni Mia nane na Themanini (882,000,000/=) hivyo tunayoimani kubwa wananchi wataongeza mapato kupitia mifugo yao kwa kuuza maziwa na ufugaji utaongezeka zaidi kwani wengi wao walikuwa wanachukia ufugaji kutokana na changamoto ya maji."
Akisindikiza ujumbe huo maususi wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Butiama Marwa Siagi, amewatoa hofu wananchi wa kata hiyo na Wilaya Butiama kwa ujumla kupuuza mambo ya mitandaoni yanayoenezwa na baadhi ya watu kwa masilahi yao binafsi, na badala yake wawe na imani na chama na wawatumie wawakilishi wao vyema ili kuzidi kusogeza kurudumu la maendeleo mbele kwani Chama kiko kazini kutekeleza Ilani yake.
"Kadiri huduma za kijamii zinavyozidi kutekelezwa ndivyo wananchi wanavyozidi kutamani, ukitekaleza Kata A Kata B pia wanawiwa na wao kutekelezewa hivyo ni vyema kuwa na subira Pesa zinatafutwa na zinatolewa kila kata na Wilaya ndani Nchi yetu tuweni watulivu tuzidi kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Taifa letu na jamii zetu tuyapuuze mambo ya mitandaoni na vijiweni yaliyojaa uchochezi na chuki,Serikali kupitia viongozi wake kuanzia ngazi ya Kata hadi Taifa kwa kushirikiana na Chama tukiwemo na sisi wawakilishi wenu tupo kazini"amesema Sagini.
Hakuna maoni