HOT News

WAZEE WAMPA BARAKA MBUNGE KWA UTENDAJI BORA

 




Wazee wa kata ya Nyakanga wilayani Butiama wampa baraka mbunge wa Jimbo la Butiama kwa kumfanyia maombi kupitia viongozi wa mathehebu mbalimbali ndani ya kata hiyo na kuweka kumbukumbu ya kudumu kwa kuipa jina shule  ‘Jumanne Sagini sekondari’ ambayo mwanzo iliitwa ‘Nyabange sekondari’ kama sehemu ya shukrani ya juhudi zake  za ujenzi wa shule hiyo ambayo ilikwama kwa miaka kadhaa.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wa kata hiyo mzee maarufu Marwa washasha  alitoa shukrani za dhati  kwa mbunge kwa kutatua kigugumizi kilichokuwa kikikwamisha  ujenzi wa shule hiyo ambayo sasa inaenda kuwapunguzia mwendo Watoto wa kata hiyo kwani walikuwa wakitembea umbali wa kilomita nane kwenda Kemoramba sekondari jambo ambalo lilichangia Watoto wengi kutofaulu vizuri katika masomo yao na wengine kushindwa kuhitimu.

Aidha katibu kata  wa chama  cha mapinduzi kata ya Nyakanga Japhet Changarawe Mashaga  amempongeza mbunge kwa juhudi zake za kiutendaji hasa katika sekta ya Elimu ndani ya jimbo  na wilaya ya Butiama,jambo ambalo ni  chachu ya kuongeza ufaulu kwa Watoto na namna anavyohamasisha walimu  kufanya kazi kwa ueledi hii ni ishara ya kuongeza ufaulu na kufuta ziro mashuleni.

Hata hivyo Mbuge wa jimbo hilo la Butiama Jumanne Sagini aliwashukuru wazee hao kwa kuutambua mchango wake na kuwahiidi kuendelea  kushirikiana nao na kuendelea kutekaleza ilani ya chama cha mapinduzi kama ilivyopangwa,na  kuwasihi wazee kujitokeza kuhesabiwa wakati huu wa sensa kwani bila kupata takwimu kamili serikali haitaweza kujua ni watu wangapi wanatakiwa kupewa huduma hivyo ni vyema wao na familia zao wajiandae kuhesabiwa kwa maendeleo ya kata yao na nchi kwa ujumla.


                FOR MORE INFORMATION VIST US ON YOUTUBE @NEVILLADIGITALTV

Hakuna maoni