TAKUKURU MKOA WA MARA IMEFUATILIA UTEKELEZAJI MIRADI 24 NA KUBAINI MIRADI MITATU ILIYOTEKELEZWA CHINI YA KIWANGO.
Na Neema Kobiro,
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoani
mara wameweza kufuatialia miradi 24 inayotekelezwa mkoani humo inayogharimu kiasi cha sh Billion kumi na nane,Million mia tano sabini na nane
laki tatu una elfutisa,Mie nne themanini na tano shs.18,578,309,485 katika
sekta za Afya, Barabara,Maji na Elimu.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu mkuu wa Takukuru Mara bwana Athony Gang’olo amesema kufuatia ufuatiliaji huo wameweza kubaini miradi mitatu iliyotekelezwa chini kiwango ambayo ni;-
i, Ujenzi wa chumba cha wagonjwa wa dharura hosptali ya halmashaur ya mji wa tarime wenye thamani ya sh 300,000,000/= kwa kuchelewa kutekelezwa na baada ya kufanya ufatiaji umeanza kutekelezwa.
ii, mradi wa maji katika Kijiji cha Robanda Wilaya ya Serengeti wenye thamni ya sh 685,151,776/= umebainikwa kuwa kinyume na sheria na taratibu za manunuzi.
iii, Mradi
waujenzi wa vyumba vya madarasa hauna ubora wa scheming haikufanyika.
Aidha katika kipindi cha cha Aprili – Juni jumla ya
malalamiko 106 waliyoapokea kati ya hayo
malalamiko 79 yalihusu vitendo vya Rushwa na 27 hayakuhusishwa na Rushwa
malalamiko 27 ambayo hayakuhusishwa na rushwa walalamikaji walipatiwa ushauri na kuelimishwa na mengine matano
yalihamishiwa idara zingine kwa kupatiwa ufumbuzi na malalamiko 79 yanahusu rushwa
yanaendelea kufanyiwa kazi kwa kukusanya nyaraka za Ushahidi kwa kuwahoji
mashahidi na watuhumiwa kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa
namba 11ya mwaka 2011.
Sambamba na hayo Takukuru
imejipanga katika kipindi cha Julai-Septemba 2022,kuongeza nguvu zaidi
kwa kuzuia vitendo vya rushwa na kuimarisha miundombinu ya ukusanyaji
habari ili kubaini vitendo vya rushwa kabla havijafanyika.
Hakuna maoni