INNOCENT BASHUNGWA HALMASHAURI 100 ZAKUSANYA MAPATO KWA ASILIMIA 100 NCHINI
Waziri wa nchi ofisi ya rais TAWALA za Mikoa na Serikali za Mitaa OR -TAMISEMI Mhe Bashungwa amesema katika mwaka wa fedha 2012-2022 Halmashauri 100 zimekusanya mapato ya ndani kwa asilimia 100 au zaidi ya lengo la mwaka.
Ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kuhusu mapato na matumizi ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2012-2022,Leo Agost 2,2022 Jijini Dar-es-salaam.
Aidha Bashungwa amesema Halmashauri 78 zimekusanya kati ya asilimia
80 mpaka 99na halmashauri 7 zimekusanya kati ya asilimia 58 hadi 79 na
zilizoweza kufikia malengo zimeongezeka kutoka Halmashauri 57 katika mwaka wa
fedha 2020-21 na kufikia halmashauri 100 kwa mwaka 2021-2022.
Akiendelea kutoa ufafanuzi wa ukusanyaji wa mapato ameitaja Halmashauri ya wilaya ya Kibaha kwa kuongoza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 247 ya makisio yake yam waka ikifuatiwa na Halimashauri yaWilaya ya Mlele iliyo na asilimia 185 huku Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro asilimia 158.
Sambamba na hayo amesema Halmashauri 4 zimekusanya chini y ash Billion 1 ambapo Halmashauri ya wilaya ya Bumbuli imekuwa ya mwisho kwa kukusanya sh Million 599.7
Hakuna maoni