HOT News

MKUU WA MKOA WA MARA MEJA JENERARI SULEIMAN MZEE AWASILI OFISI ZA CHAMA KUPOKEA BARAKA NA KUKABIDHIWA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

 

Mkuu wa mkoa wa Mara awasili ofisi za chama Mkoani humo na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama wakiongozwa na katibu wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Mara Bwana Langaeli Akyoo.

Akizungumza na kumkabidhi ilani ya chama cha mapinduzi katibu wa chama mkoa  wa Mara amemuomba kuwa huru katika utendaji kazi wake kwani wananchi na wakazi wa  Mkoa wa Mara si wabaya kama wanavyozungumzika huko ila ni watu wanaopenda ukweli na haki  hivyo ni vyema  kuitekeleza ilani ya Chama  kama ilivyopangwa.



Aidha katibu amemuahidi kumpa ushirikiano wa hali ya juu mara tu atapohitaji msaada kwa upande wa chama pindi tu anapokwama.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa ametoa shukrani za dhati kwa Chama kwa mapokezi yao mazuri na kuahidi kwenda sambamba na  viongozi wa chama ikiwa nisehemu ya kutimiza yale yote yaliyokusudiwa na chama kupitia ilani.



Hata hivyo mkuu wa Mkoa  amelimaliza kwa kutoa msimamo wake wa kiutendaji ''Mimi ni mtu wa kazi na katika utendaji wangu wa kazi napenda kuwa mbunifu  kwa kila hali hata kama nitakuwa sina pesa ya kukamilisha mradi  flani au jambo flani katika shughuli zangu za kiutendaji napenda kutumia njia mbadala kutatua hivyo napenda kuwaomba viongozi wenzangu kuongeza ubunifu katika kazi kwa maendeleo ya mkoa wa Mara.’’

Hakuna maoni