UPANDAJI WA MADARAJA,MKOMBOZI WATUMISHI WILAYANI BUTIAMA.
Watumishi Halmashauri ya wilaya ya Butiama mkoani Mara, wametoa shukurani za dhati kwa Rais Samia kwa kuwapandisha daraja kutoka kimo cha chini hadi mishara ya kati kwani upandashaji huo utaweza kuwapelekea kukabiriana na hali ya uchumi wa Nchi wa sasa.
Wakizungumza na waandishi wa habari wilayani humo mpja ya
watumishi hao,Agnes Kisuka amesema takribani miaka saba watumishi hao hawakuweza
kupata ongezeko la aina yoyote hivyo kupitia uongozi wa Rais Samia zaidi ya
asilimia 23% zimeweza kuongezwa katika mishahara ikiwemo kuwapandisha daraja
watumishi wa kimo cha chini cha mishahara.
Ongezeko hilo la mishahara limeweza kupelekea watumishi kwenda kuchukua mikopo katika mabenki kulingana na mishahara yao ambavyo nitofauti na ilivyokuwa awali pia weledi na ufanisi umeweza kuongezeka kiutendaji.
Leopold Constantine ambae ni Afisa maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Butiama nae ametoa shukrani zake kwa raisi Samia kwa kutujali kwa kutuletea pesa za kutosha kuia OC ambayo ni ruzuku ya uwendeshaji wa kazi za ofisi huko nyuma tumekuwa tukipewa pesa kodogo tofauti na sasa Rais wa awamu ya sita ametupatia pesa za kutosha hivyo tunampongeza sana na tunamuahidi tutazididi kufanya kai na hatu
Constantine aliendelea kwa kusema kuwa kwa sasa makundi yote ambayo yananufaika
na mkopo hivi sasa watanufaika na huduma hiyo ipasavyo kutokana na namna Rais
alivyoijali idara hiyo asilimia kumi ya mkopo wa Akina mama,Walemavu,Vijana na
wao kama watendaji wanao uhakika wa kuwatembelea wanufaika hao kwani
amewawezesha pesa ya kutosha tofauti na huko nyuma ilikuwa ni ngumu watumishi
kuwafikia wanufaika kwa kukosa uwezesho.
Hakuna maoni