NITASIKILIZA MALALAMIKO YOTE NA KUYAFANYIA KAZI HAKUNA UCHAGUZI WA MAELEKEZO.
Naibu katibu mkuu bara Bi Riziki Kigwanga amewatoa wasiwasi jumuia ya akina mama UWT Mkoa wa Mara katika uchaguzi unaondelea ndaniya chama na jumuia zake kuwa kila mtu ana haki ya kugombea nafasi anayoona anaweza kuisimami kwa kufuata taratibu na kanuni za chama na jumuia zake.
Hayo ameyasema katika ziara yake ya kikazi inayoendelea mkoani Mara na kutembelea wilaya ya Bunda, Musoma na Musoma DC na kuongozana na viongozi mbalimbali wa jumuia ya UWT mkoani humo pamoja na Mbunge viti maaalum Ghati chomete, lengo likiwa ni kuhamasisha sensa ya watu na makazi na kuwakumbusha wanachama wa Jumuia hiyo kuchagua viongozi wenye manufaa pamoja na kutumia frusa za mikopo inayotolewa na serikali ndani ya Halmashauri ili kujikwamua kiuchumi.
Aidha Bi Riziki alisema kuwa chama hiki ni cha enzi na enzi hivyo ni vyema kukindeleza kwa kudumisha umoja wa kiutendaji na kuendelea kutoa elimu juu ya jumuia ya wanawake UWT ili kusaidia kukuza Jumuia na kuongeza wanachama wapya kwa manufaa ya baaadae.
Pia alitoa pongezi kwa mbunge viti maalum mkoa wa Mara Mh Ghati Chomete kwa kuwawezesha wanawake kwa kuwafungulia akaunti ili waweze kupata mikopokatika Halmashauri zao na kuwakumbusha kuweka malengo mazuri ya pesa hizo na si kwenda kuzitumia kwa matumizi ya kuvaa,kula na sitarehe zitazowapelekea kushindwa kurejesha mikopo yao na kuwaingiza matatizoni.
Hata hivyo alimazaliza kwa kuwashukuru wanachama wa Mkoa wa Mara kwa mapokezi mazuri na kuwaomba washiriki vyema zoezi la sensa ya watu na makazi ili kusaidia serikali kupata takwimu sahihi zitakazosaidia kuleta maendelea katika sekta zote ndani ya mkoa wa Mara.
Hakuna maoni