HOT News

VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA RABUOR WAPINGWA MSASA JUU YA UONGONZI BORA.

VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI  KATA YA RABUOR WAPINGWA MSASA JUU YA  UONGONZI BORA.



Viongozi wa chama cha mapiduzi ngazi ya kata na mashina kata ya Rabuor iliyopo Wilayani Ryolya mkoani Mara wapewa seminar juu uongozi na namna wanavyotakiwa kufanya kazi za chama cha mapinduzi kwa ueledi katika kipindi chote watakapokuwa maradarakani.

Akifungua serminar hiyo kaimu katibu wa chama cha mapinduzi mkoa mara Bw Burhani Abdul Ruta ambae ndie aliekuwa mgeni rasmi katika seminar hiyo amewaomba viongozi hao wa kata ya Rabour kufanya kazi kwa ueledi na kuendelea kukijenga chama katika misingi iliyo bora na kuwa wao ndio mwanzo wa chama katika jamii zao.

Nae diwani wa kata hiyo mh Gerald Ng'ong'a  ambae pia ni mwenyekitiwa Halmashauri ya Wilaya ya Rolya ameeleza lengo la seminar hiyo ni kutaka kuwaelekeza viongozi hao  hao namna ya kuyaendesha majukumu yao kila mmoja kwa nafasi yake.

Aidha Ng'ong'a amesema  kuelekea katika chaguzi za viongozi wa mtaa ni vyema viongozi hao waendelee kukijenga chama kwa kushirikiana na serikali  kwa kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi na kuondoa migogoro isiyo na tija ndani ya chama.

Pamoja na hayo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi  kata ya Rabour bwana John Odonda kwa niaba ya waseminishwaji wote amemshukuru Diwani wa kata hiyo kwa kuwaandalia Seminar hiyo kwani imewasaidia kuwajengea uwezo wa kiutendaji kwani miongoni mwa viongozi ni wapya hivyo itawasidia kiutendaji.



  


Hakuna maoni