MASHABIKI WA SIMBA WAFANYA USAFI
Na Shomari Binda.
Mashabiki wa Simba tawi la Machinjioni wamejitokeza kwa wingi
kufanya usafi kwenye eneo lao ikiwa ni kilele cha wiki ya simba.
Katibu wa tawi hilo,Bwire Misiro ,amesema katika kuadhimisha
siku hiyo wameamua kufanya shughuli ya kijamii kwa kufanya usafi.
Amesema mazingira safi yanaepusha magonjwa hivyo jamii
inapaswa kuzingatia usafi kwa afya bora.
Bwire amesema usafi ni suala endelevu na kutoa wito kwa wanasimba
kwa kila tawi na mashabiki wote kushiriki kikamilifu katika kudumisha usafi.
Nae msemaji wa simba tawi la machinjioni Masatu Kawawa,amewashukuru
mashabiki wa simba kwa kujitokeza kwa wingi kukamilisha zoezi na kusema
wataendelea kuhamasisha jamii kushiriki vyema kutunza mazingira kwa kufanya
usafi.
Hakuna maoni