CHODAWU WABAINI CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI SEKTA BINAFSI MKOANI MARA
Chama cha wafanyakazi Sekta binafsi wa Hifadhi,mahotelini,majumbani na
huduma za kijamii na ushauri CHODAWU wamebaini changamoto za wafanyakazi walioajiliwa sekta binafsi kutowatendea haki za kiutumishi na waajili wao.
Akizungumza na waandishi mapema leo katika ofisi za CHODAWU mkoa mara, katibu wa chama hicho mkoa humo Bw;Machunde Mauma Raymondi,amesema
moja ya changamoto kubwa wanazokabiliana nazo wafanyakazi ni kufanya kazi bila Mikataba baina yao na
waajili hali inayopelekea wanyakazi wengi kupoteza haki zao za msingi.
‘‘Waajili wengi hawawapi wafanyakazi wao mikataba na
hawawawekei wafanyakazi wao pesa NSSSF na kuwanyima muda wa likizo hali inayopelekea
wafanyakazi katika sekta binafsi kushindwa kufanya kazi zao kwa utulivu,na pindi mwajiliwa inapomlazimu kwenda likizo mwajili humwajili mtu mwingine hali inayopelekea upotevu
wa haki za mfanyakazi na bahati mbaya wengi wao huwa hawana mikataba.’’
Aidha amewaomba wananchi wakazi wa mkoa wa Mara walioajiliwa katika sekta binafsi kujiunga na chama cha CHODAWU kwani chama kinachoshughulika na kutetea masilahi ya wanyakazi na hata wanaofanya kazi za majumbani,.
Hata hivyo alihitimisha kwa kutoa wito kwa waajili wote kuwaruhusu wajiliwa wao kujiunga na CHODAWU kwani Chodawu inashughulika na kuwashauri na kuweka usawa kati ya mwajili na mwajiliwa na si vinginevyo.
Hakuna maoni