UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM TARIME RORYA LAMKOSHA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM TARIME RORYA LAMKOSHA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Na Neema Kobiro.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini Atoa pongezi kwa mkuu wa Jeshi la polisi kanda maalum Tarime -Rolya kwa kazi nzuri na yenya kasi ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya Jeshi kanda maalum linalojengwa Mji wa kiserikali Bomani Mjini Tarime mkoani mara ujenzi utakaogharimu kiasi cha sh .Bilioni 1.5
Akisoma taarifa kwa niaba ya
kamanda wa polisi kanda maalum Ahia
Rumisha, amesema uwepo wa makao makuu ya Jeshi la polisi itakuwa ni msaada
mkubwa kwa wananchi na Jeshi kwa ujumla kutokana na huduma zitakazotolewa.
Aidha katika ziara hiyo Naibu waziri wa mambo ya Ndani alitembelea na kukagua kituo cha polisi cha Kegonga kata ya Nyanungu kilichojengwa mabati juu chini alimaarufu kama fulusuti,na kubaini changamoto za kiutendaji kwa asikari wa kituo hicho ikiwemo ukosefu wa usafiri.
"Nimefurahi kufika katika kituo hiki na nimeziona changamoto zinazowakabili asikari wetu pamoja na wannchi wa maeneo haya nina imani tutalifanyia kazi kiserikali ili ujenzi wa kituo hiki uanze kwa haraka ili kuleta amani zaidi kwa wanachi na askari wetu”Sambamba na hayo Mbunge wa Jimbo
la Tarime Vijijini mhe Mwita Waitara
aliwasili katika ziara hiyo ya Naibu waziri wakati akikagua kituo hicho cha
polisi cha Kegonga kata ya Nyanungu kilichopo ndani ya jimbo lake na kuahidi
kutoa kiasi cha sh.10,000,000/=na kuwaomba wanchi kuonyesha juhudi za binafsi
kwa kujitoa kushiki kukamilisha ujenzi wa kituo hicho pindi utakapoanza.
Pamoja na hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ametoa pongezi kwa Vikosi vya ulinzi na Usalama pamoja na viongozi wa serikali waliopo mpkani mwa Tanzania kwakushirikiana vyema na wenzetu wa nchi jirani ya Kenya kwa manufaa ya Taifa letu.
Hata hivyo Naibu waziri Sagini aliwasihi vijana wa kituo kidogo cha forodha cha Kogaja wanaofanya kazi za bodaboda katika mpaka huo kufuata taratibu za kusajili vyombo vyao vya usafiri kwa taratibu za nchi ya Tanzania ili kuondokana na usumbufu pale wanapotumia pikipiki zenye usajili wa namba za nchi jirani ya Kenya kwani hii inaweza kuwapa tabu pale wanapokutana na asikari wa Tanzania na kuwaomba asikari hao kutoa elimu kwa vijana hao mara kwa mara.
Hakuna maoni