HOT News

NISINGEPENDA MTU AU WATU KUTUMIA JINA AU NAFASI YA MBUNGE KWA UCHAGUZI UNAOENDELEA NDANI YA CHAMA,MBUNGE JUMANNE SAGINI.

 

NISINGEPENDA MTU AU WATU KUTUMIA JINA AU NAFASI YA MBUNGE KWA UCHAGUZI UNAOENDELEA NDANI YA CHAMA,MBUNGE JUMANNE SAGINI.

Mbunge wa jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini amewaomba wanachama wa chama cha mapinduzi kutomhusisha kwa manufaa binafsi ya mtu au watu katika uchaguzi unaoendelea ndani ya chama cha mapinduzi kwani yeye ni mbunge wa watu wote na si mbunge wa mtu au watuflani.

    Ameyasema hayo katika kikao cha halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya butiama.

Aidha Sagini amewaomba wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea kuwapa kipaumbele vijana kwa kuwafamisha mengi na mema yanayofanywa na chama cha mapinduzi na kuwasihi wajitokeze kwawingi kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama ili kuendelea  kukiimarisha chama kwa manufaa ya vizazi vijavyo.


Sambamba na hayo mbunge aliwaomba viongozi wa chama kuanzia ngazi ya shina mpaka wilaya kuwa wamoja nakushirikiana kwa pamoja ili kuzidi kuijenga Butiama kimaendeleo zaidi na kuongeza kuwa Niliahidi kujenga kiwanda hapa Butiama na sasa nimenunua mashine kwaajili ya kutengeneza sabuni na hivyo basi nitakabidhi uongozi wa chama ili kuwasaidia vijana wetu kupata ajira na kuongeza pato ndani ya chama chetu na ndani ya jimbo letu la Butiama.


Hata hivyo katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Butiama ndugu Hamisi Mkaruka Kura amewaomba wanachama kuwawatulivu kipindi hiki cha uchaguzi kwani hakuna atakaetendewa kinyume uchaguzi utafanyika kwa kufuata taratibu na kanuni za chama.

Hakuna maoni