HOT News

MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA YA RUFIJI KUBORESHA MAKAZI YA WALIMU NA VYOO VYA WANAFUNZI



      Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ya Rufiji John Lipesi Kayombo         katikati akiwa katika harakati za ukaguzi wa Miradi


Na mwandishi Wetu,

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji John Lipesi Kayombo amefuta kilio Cha makazi duni  kwa kuahidi kujenga nyumba nne za Walimu pamoja na matundu 24 ya vyoo kwa Walimu wa Shule ya Msingi Mbwara Kata ya Mbwara ili kuboresha makazi ya Walimu pamoja na vyoo vya Wanafunzi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu.

 

Ameyasema hayo baada ya kuguswa na mazingira magumu ya Walimu na Wanafunzi aliyoyaona wakati alipotembelea shule hiyo Julai 24.2022 akiwa katika ziara yake ya siku tatu ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani pamoja na ruzuku toka Serikali kuu. 


"Mhe. Rais anafanya kazi kubwa kuboresha miundombinu ya elimu na sekta nyingine Nchini zikiwemo nyumba za Wafanyakazi na maslahi yetu,Sisi wasaidizi wake Tutaleta fedha mapema mwezi ujao kwa ujenzi wa nyumba nne za Walimu pamoja na matundu 24 ya vyoo vya Wanafunzi kukidhi mahitaji ya shule. Tumepunguza matumizi ya ofisi na kupeleka fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo Hadi Sasa tumeshaanza miradi ya ujenzi wa Nyumba za Walimu ikiwemo shule ya Msingi Siasa, Shauri moyo na Nyakipande kwa mapato ya ndani". Alisema Kayombo

 

Ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji katika utekelezaji wa vipaumbele vyake kwenye sekta ya Afya na Elimu hususani katika kutatua kero za ukosekanaji wa Jengo la mionzi, ujenzi wa Jengo hilo upo katika hatua ya umaliziaji na kuwa tayari imeshapokea mashine mpya ya mionzi ambapo huduma hiyo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Katika hatua nyingine akiendelea na ziara yake ya ukaguzi wa miradi Shule ya Sekondari Mohoro ameagiza kufanyika ukaguzi maalumu katika Jengo la bwalo la chakula linalotekelezwa kwa kiasi Cha shilingi milioni 100,  ili kubaini matumizi ya fedha yaliyofanywa katika mradi huo.


Hata hivyo ameendelea kutoa msisitizo kwa wasimamizi wa miradi kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo kwa kuzingatia taratibu huku akizitaka kamati za ujenzi kuhakikisha zinawajibika ipasavyo na kuwa hatavumilia ikiwa kamati zitajihisisha na uhujumu wa miradi hiyo.

 

Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji inatekeleza miradi zaidi 152 ikiwemo miradi ya Afya na Elimu katika Kata zote 13.

___________________________________________________________________________________

       FOR MORE INFORMATION VIST US ON YOUTUBE @NEVILLADIGITALTV

Hakuna maoni