HOT News

MKUU WA MKOA WA MARA AMEWATAKA WARATIBU WA SENSA MKOA HAPO KUHAKIKISHA MAKARANI WOTE WA SENSA WANAPATA MALIPO YAO KWA WAKATI.

 


                    Ally Hapi, Mkuu  wa Mkoa wa Mara

Na Neema Kobiro,

Mkuu wa mkoa wa mara ndugu Ally Hapi amewataka waratibu wa sensa mkoani humo kuhakikisha makarani wote walioteuliwa kusimamia zoezi la sensa kuanzia ngazi ya wilaya mpaka kitongoji wanapata malipo yao kwa wakati ili kuwapa uwepesi wa kiutendeji pindi wanapokuwa katika zoezi la ukusanya takwimu kwa kila kaya.

Hayo amesema katika kikao cha kufunga mafunzo kwa waratibu wa sensa ngazi ya mkoa yaliyofanyika kwa siku 21 mkoani mara kwa waratibu 296.

Aidha  amewaagiza waratibu kuwasimamia vyema makarani watakaokuwa wakikusanya takwimu za sensa kuwa waadilifu kwa mavazi, lugha Rafiki na kuepuka matumizi ya vinywaji vikali pindi wanapokuwa  kazini.

Pia amewasihi wananchi hususani vijana kwa waliokosa nafasi za zoezi la ukusanyaji takwimu kipindi hiki cha sensa kuwa watulivu kwani serikali haikuwa inatoa ajira rasmi kama jamii inavyotafasili ila walihitaji watu wenye vigezo watakaosaidia serikali kukamilisha zoezi la sensa.

Sambamba na hayo mkuu wa mkoa ametoa pongezi kwa kamati za sensa kazi ya mkoa na ngazi za wilaya zote kwa  kufanya kazi nzuri .

 

___________________________________________________________________________________

💥FOR MORE INFORMATION VIST US ON YOUTUBE @NEVILLADIGITALTV

Hakuna maoni