"NINAYO IMANI MAGWEIGA MNANKA SAMO ANGEITUMIA FURSA HII" MUNGU AMPE PUMZIKO JEMA.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Butiama, ambaye
pia ni Naibu Waziri Wa Mambo Ya Ndani ya Nchi Mh Jumanne Sagini, alipofika
Msibani kwa mfanyabiashara mahiri na mpenda maendeleo bwn Magweiga Mnanka Samo, na kusema kufuatia
uwepo wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere na Chuo cha ufundi stadi VETA .
Butiama sasa inahitajika kupata wawekezaji kwa ajili ya
kufanikisha makazi ya wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na vyuo hivyo, licha ya
Serikali kujenga Hostel itakayochukua
wanafunzi mia nane (800) kadhaa ndani ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere bado kunakuwa na
upungufu mkubwa wa makazi ya wanachuo kwani chuo kitakachochukua wanafunzi zaidi ya Elfu Nne( 4000)kwa uwiano huo tunaona bado kunauhitaji mkubwa wa Nyumba, hivyo ni vyema wana Butiama kutumia frusa
hiyo kujenga nyumba kwa ajili ya biashara na kuanza kuweka mikakati thabiti ya
kuanzisha Biashara mbalimbali ili kukidhi mahitaji kwa wanavyuo na ikiwa ni
sehemu ya ongezeko la ajira kwa wana Butiama.
“Nina imani bwana Magweiga angekuwepo lazima angeitumia
fursa hii kwani alikuwa mpenda maendeleo”amesema Sagini.
Sagini alifika
msibani hapo akiwa ameongozana na viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi Wilaya
ya Butiama.
Aidha Sagini alitoa pole nyingi kwa familia na kuwasihi kuwa
wavumilivu na kufuata taratibu zote
mirathi ili kuepuka migongano na mivurugano kwa familia hiyo, hii
itasaidia familia kuendelea kuwa imara na kyaendeleza yote aliyokuwa akiyafanya
na kuyasimamia Baba au Kaka wa familia ambae marehemu Magweiga Mnanka Samo.
Aidha Bi Christina
Ndengo Nyahurya ambae ni Mwenyekiti wa chama cha Sauti ya UmmaSAU,Akizunguma
kama muwakilishi wa vyama vingine vya kisiasa aliiwasihi Wazazi na Walezi
kuwalea watoto katika maadili ya kumpendeza mungu ili baadae wapatikani akina
Magweiga wengine kwa ajili ya masilahi mapana
ya Taifa letu na jamii zetu na kuwaomba wanafamilia kuhakikisha
wanasimamia na kukamilisha ujenzi wa
Shule na Kanisa aliokuwa ameanzisha bwana Magweiga kijijini kwao
Kongoto.
Hakuna maoni